ENG. KUNDO AMPIGIA SALUTI RAIS DK.SAMIA KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO.

 

MBUNGE wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi Kundo Mathew (katikati) akiongea na Wananchi wa Kata ya Gibishi wiayani Bariadi Mkoani Simiyu (hawapo pichani) juu ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020/2025.


Na Costantine Mathias, Bariadi.


MBUNGE wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi Kundo Mathew amempongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo nchini hususani Jimbo la Bariadi Mkoani Simiyu.


Amesema kuwa, serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imesimamia Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kiasi kikubwa na kwamba imetekeleza miradi mingi ya Maendeleo katika sekta za Elimu, Afya, Maji, Umeme, Barabara, Mawasiliano na miundombinu mingine na kuwarahisishia huduma wananchi.


Mhandisi Kundo ameyasema hayo leo, kwenye Mikutano Maalumu wa kuwasilisha Utekelezaji waIlani ya CCM katika kata za Gibishi na Nkindwabiye huku akitumia fursa hiyo kiwashukuru wananchi kwa kuendelea kuwaunga mkono viongozi wa CCM.


"Nitumie fursa hii kumshukuru Rais Dk. Samia kwa kutupendelea na kutupatia fedha za miradi ya Maji, tumepokea zaidi ya shilingi Mil. 300 ambazo tumenunua pampu 100 ambazo tumeanza kugawa katika vijiji 84...tunamshukuru kwa kutupatia fedha za Maendeleo hususani Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria". Amesema.


Akiwa kwenye mwendelezo wa ziara yake, Mbunge Kundo amekabidhi pampu tatu zenye thamani ya shilingi Mil. 10 ambazo zitafungwa kwenye maeneo yenye visima vya Maji ili kuwapatia wananchi Maji safi na salama.


Katika hatua nyingine, Mbunge Kundo amekabidhi mipira 19 na jezi pea tano kwa ajili ya kumuunga mkono Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika kukuza sekta ya michezo na kuibua vipaji kwa vijana.


Akiwa kwenye kata ya Nkindwabiye, Mbunge Kundo amekabidhi pampu za Maji 4, mipira 19 na jezi pea tano kwa ajili ya kata nzima ya Nkindwabiye na Matawi ya Nkindwabiye, Songambele, Halawa na Damidami



Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira, Mhandisi Moses Mwampunga amesema wamekamilisha kazi waliyoagizwa ya kuchimba kisima kirefu katika Gibishi na kwamba pampu hizo zitawarahisishia wananchi kupata Maji safi na salama.



"Kabla ya kujenga miundombinu, tumeamua kila eneo wapate pampu moja moja, umeagiza tuweke kila Kijiji, tumeleta ziko hapa leo na zitaanza kufungwa kesho tunaomba vijiji watupe visima hata tuanze kufunga pampu za Maji" amesema Mhandisi Mwampunga.


Mwisho.

























Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم