Maadhimisho siku urithi wa Dunia kufanyika kesho Mara.

Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti Stephano Msumi akizungumza na waandishi wa Habari makao makuu ya Hifadhi hiyo (Sorenera) kuelekea maazimisho ya siku ya urithi ya wa Dunia ambayo kitaifa yanafanyika kesho (leo) Wilayani Serengeti Mkoani Mara (Picha na Derick Milton)

Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti Stephano Msumi akizungumza na waandishi wa Habari makao makuu ya Hifadhi hiyo (Sorenera) kuelekea maazimisho ya siku ya urithi ya wa Dunia ambayo kitaifa yanafanyika kesho (leo) Wilayani Serengeti Mkoani Mara (Picha na Derick Milton)


Na Derick Milton, Serengeti.


Maazimisho ya siku ya urithi wa Dunia kitaifa yatarajiwa kufanyika kesho Mkoani Mara katika Wilaya ya Serengeti, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evance Mtambi.


Akitangaza uwepo wa maazimisho hayo kwa waandishi wa Habari leo, Mkuu wa Hifadhi ya taifa ya Serengeti Stephano Msumi amesema kuwa maazimisho hayo yatahudhuriwa na wakuu wa maeneo ya urithi wa dunia nchini pamoja na wakuu wa maeneo ya uridhi wa taifa.


Amesema kuwa kuelekea maazimisho hayo kauli ni “Majanga na migogoro ni tishio la urithi wa dunia” lengo likiwa kuikumbusha jamii na wadau katika umuhimu wa uhifadhi na kulinda urithi wa dunia.


Ameeleza kuwa kwenye maazimisho yatakuwepo maonyesho mablimbali ya maeneo ya uridhi wa dunia, maeneo ya urithi wa taifa, pamoja na maonyesho ya tamaduni mbalimbali.


“ Uwepo wa maazimisho haya lengo lake kubwa ni kuwaonyesha watanzania vivutio mbalimbali vya utalii ambavyo vipo katika urithi wa dunia pamoja na kuwaelimisha umuhimu wa kuvitunza na kuvilinda,” amesema Msumi.


Naye mwakilishi wa Tume ya taifa ya Shirika la umoja wa mataifa la elimu sayansi na utamaduni (UNESCO) Anajoyce Tadeo amesema kuwa shirika hilo linaridhishwa na juhudi za serikali ya Tanzania katika kulinda, kuhifadhi maeneo yote ambayo yapo katika urithi wa dunia.


Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post