MAPOKEZI YA MBUNGE YAFUNGA MJI WA NKOLOLO, AKIWASILISHA ILANI YA CCM.

Wakazi wa Nkololo wakimpokea Mbunge wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi Kundo Mathew aliyefika kwa ajili ya kufanya Mkutano Maalumu wa kuwasilisha Ilani ya CCM 2020/2025.




Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.


MAPOKEZI ya Mbunge wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi Kundo Mathew yamekuwa ya aina yake wakati Mbunge huo akiwasilisha kata ya Nkololo kwa ajili ya kuwasilisha Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020/2025.


Wanachama wa CCM pamoja na Wananchi wengine kutoka Kata ya Nkololo, walimpokea Mbunge huyo akitokea kata ya Mwadobana na kumbeba kwenye bajaji ya mizigo (Guta) ambapo mapokezi hayo yalisimamisha shughuli za Biashara na usafiri katika Mji huo unapokuwa kibiashara.


Akizungumza kwenye Mkutano wa kuwasilisha Ilani ya CCM kwenye viwanja vya Kanisa Katoliki Nkololo, Mbunge huyo amewapongeza wananchi hao kwa mapokezi mazuri huku akiwasisitiza kujiandaa na Uchaguzi Mkuu kwa ajili ya kuchagua Madiwani, Mbunge na Rais.

Mbunge huyo amewataka Wananchi kufaanya Uchaguzi amani na kuendelee kuhubiri amani kwani pasipo kuwa na Amani hakuna Maendeleo, huku akisisitiza kuwa kipaumbele cha Rais Dk. Samia ni Amani.


Ameongeza kuwa, serikali ya Dk. Samia imetekeleza miradi ya Maji, Barabara kwa kiwango cha lami pamoja na taa za Barabara ambapo wafanyabishara na Wananchi wananufaika nazo.

Kata ya Nkololo inayojumuisha vijiji vya Mwamoto, Chungu cha Bawawa, Bubale, Nkololo na Mwabadimu, kila kijiji kilipokea mipira 4 ya miguu na jezi 1, na hivyo kufanya jumla ya mipira 20 na jezi 5.


 Aidha, kwa ajili ya timu ya kata, mipira 3 na jezi 1 ziliongezwa, kata hiyo pia imenufaika kwa kupatiwa pampu 5 za maji kwa vijiji vyake, jambo ambalo litaboresha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi._


Mbali na misaada hiyo, Mhandisi Kundo ametumia Mkutano huo kutoa taarifa muhimu kwa wananchi kuhusu mabadiliko ya kiutawala yaliyofanyika katika Jimbo la Bariadi ambalo limegawanywa na kupata majimbo mawili.


Ameeleza kuwa Jimbo hilo limegawanywa na kwamba yeye (Mhandisi Kundo) atagombea Ubunge wa Jimbo jipya la Bariadi Vijijini katika uchaguzi mkuu ujao kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Mwisho.

















Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم