Na Costantine Mathias.
MWANDISHI wa Habari wa kituo cha Azam Tv Mkoa wa Simiyu, Rehema Evance ameibuka mshindi wa Tuzo za Samia Kalamu Award zilizokuwa zinafanyika Masaki Dome, Dar Es Salaam huku Rais Dk. Samia akiwa Mgeni Rasmi.
Tuzo hiyo ambayo imekabidhiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo kwa niaba ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.
Tuzo hizo zinafanyika Kwa mara ya Kwanza nchini ambazo zimeandaliwa na Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA.
Mwisho.
إرسال تعليق