WAFANYABIASHARA IHUSI WAMKABIDHI KUNDO FEDHA ZA KUCHUKUA FOMU YA UBUNGE.

Mbunge wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi Kundo Mathew (kulia) akipokea fedha kiasi cha shilingi Mil. 1.1 toka kwa Wafanyabiashara wa Kata ya Ihusi kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea Ubunge Jimbo la Bariadi vijijini.



Na Costantine Mathias, Bariadi.


BAADHI ya Wafanyabiashara wa kutoka Kata ya Ihusi wilayani Bariadi Mkoani Simiyu wamechanga kiasi cha shilingi Mil. 1.1 na kumkabidhi Mbunge wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi Kundo Mathew kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea Ubunge wa Jimbo hilo.


Wakizungumza kabla ya kumkabidhi kiasi hicho, Wafanyabiashara hao wamesema kuwa, wameridhishwa na Utendaji kazi wa Mbunge huyo kwa kushirikiana na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ambao wote kwa pamoja wametatua changamoto za Wananchi hao.


Tumo Majaba Mayunga, mmoja wa wafanyabiashara kutoka Kijiji cha Ihusi, amesema wameona jitihada za Mbunge huyo kutatua kero ya Barabara, Elimu, Afya, Maji pamoja na Umeme.


"Tumechanga fedha kiasi cha shilingi Mil.1,100,000/=, tunakikabidhi leo ili ukachukue fomu ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Bariadi vijiji sababu tumeona jitihada zako za kuwaletea Maendeleo wananchi...tunataka ukagombee ili uendelee kututumikia" amesema Mayunga.


Zoezi hilo la makabidhiano limefanyika jana katika viwanja vya shule ya msingi Ihusi ambapo Wafanya biashara hao wamefanya uamuzi huo baada ya Mhandisi Kundo, Kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Irani ya chama cha mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020/2025.


Mwisho.









Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم